| |
BARUA KUTOKA
DAR ES SALAAM ISLAMIC CLUB
Mheshimiwa Balozi wa Denmark
Nchini Tanzania
Dar es Salaam
Mheshimiwa,
Barua hii
inawasilisha malalamiko kwa serikali yako
kutoka kwa SHURA juu ya machapisho ya vikatuni
vinavyomuonyesha Mtukufu Mtume, (Rehema
na amani iwe juu yake) kwenye gazeti la
Denmark, Jyllads - Posten.
SHURA
inawakilisha madhehebu zote za Kiislamu
nchini Tanzania, na Dar-es-Salaam Islamic
Club ndio sekretariati yake.
Machapisho hayo sio yenye kukufuru tu katika
Uislamu bali pia ni ya kichokozi yenye kuchukiza
sana kwa sababu Mtume pia alionyeshwa kama
mtu wa vurugu.
Serikali yako kwa upande wake imeonyesha
masikitiko yake tu lakini labda ikiwa upande
mmoja na gazeti hilo kwa ngao ya Uhuru wa
Kuongea, ingawa gazeti lenyewe kwa
upande wake limeomba radhi.
Mheshimiwa,
kila uhuru unayo mipaka uliozuiliwa kwayo
unaoamriwa kibusara na murua wa msingi,
maadili na dhana iliyozoeleka ya uwajibikaji
kiasi kwamba wakati jamii inapofaidika kwa
uhuru huo, vile vile inakuwa haidhofishwi
kuhusiana na umoja na
utangamano utokanao nao.
Pale uhuru unapodhalilishwa kama utamaduni
katika nchi, serikali yake inatakiwa kuuchunga
kwa kutunga sheria. Kushindwa kwa serikali
yoyote kufanya hivyo inatwaawajibu unaolingana
kwa matokeo ya kashfa hiyo.
Utakubali bwana kwamba watu wenye namna
mbalimbali za Imani wanalazimika kutetea
maadili tofauti. Kwa suala la wafuasi wa
Uislamu, maadili yao yanahusika kwenye Uislamu
wenyewe, hususan pale ambapo Uislamu pia
ni mfumo wa maisha juu yao.
Kwa hiyo, kutegemea maadili ya kawaida ya
walio wengi, hasa kama wengi wao ni wa namna
ya kilimwengu, kuyabadilisha na maadili
ya kidini ya walio wachache, ni sawa na
kunyimwa uhuru wa kuabudu.
Kinachokera sana Mheshimiwa ni ule utambuzi-
kama ni sahihi au wa makosa- kwamba machapisho
hayo yalitiwa hamasa na chuki dhidi ya Uislamu.
Na kwa kweli, wakati huyo mhariri wa gazeti
hilo bila kutegemea, alipoulizwa katika
kipindi cha HARDTALK cha BBC kilichofanyika
Copenhagen siku ya Ijumaa kwamba itakuwa
ni sawa sawa kwake kwa hiyo, kuchapisha
katuni ya Rabbi yenye nembo ya Nazi, kama
ingeamuliwa hivyo chini ya ngao ya uhuru
wa kuongea, alionekana kulikwepa swali hilo.
Tunaona mheshimiwa, kwamba Serikali za magharibi
zina wepesi sana wa kuwahakikishia wayahudi,
na kwa kweli hivyo ndivyo ilivyo, katika
kuonekana kwa kipinga Usemiti kidogo sana
kwenye nchi zao. Panatokea hata hivyo kukosekana
kwa mazingatio kama hayo kwa Waislamu pale
wanapokosewa ambao ni wa kukusudiwa zaidi
kuliko kukosewa.
Mheshimiwa ipo haja ya kutangamanisha hali
ya kuishi pamoja kwa amani katika jamii
ya wanadamu kwa kiwango cha ulimwengu hasa
ambapo nchi yako kama nyinginezo huko
magharibi hapo zinafaidika vya kutosha,
pamoja na mambo mengine, kutokana na biashara
ya nje. Kufanikiwa zaidi juu ya soko la
wengine na kuonyesha heshima inayostahili
juu ya hisia zao za kidini lazima viende
pamoja mkono kwa mkono. Hakuna gazeti au
chombo chochote cha habari kinachoweza kuachiwa
kuvuruga uwiano huu nyeti na mazingatio
ya kulipiza.
Mheshimiwa, tumejenga hoja njema kwa serikali
yako kufanya zaidi kuliko maelezo ya juu
ya masikitiko kama itachagua kukubali ukubwa
wa kosa lililotendeka chini ya milki ya
utawala katika nchi yako.
Kwa wakati huu tunaishia hapa.
Wako mwaminifu
Balozi Abbas K. Sykes
Mwenyekiti
Dar-es-Salaam Islamic Club
S.L.P. 3125.
|