Siasa
 

ULIMWENGU WA SHIA UNAOMBOLEZA JUU YA MASHAMBULIZI YA KWENYE HARAM TUKUFU

Madhehebu ya Shia duniani kote, ynaomboleza kwa huzuni kubwa na hisia, mashambulizi
ya kupigwa mabomu kwenye Haram Tukufu iliyoko Samarrah (Kaskazini ya Baghdad ndani
ya Iraqi) ya Wajukuu na kizazi cha moja kwa moja cha Nyumba ya Mtukufu Mtume
Muhammad (s.a.w.) yaani, Imam Ali Naqi "al-Hadi", na Imam Hassan "al-Askari" (amani
iwe juu yao wote). Haram hizi Tukufu, zinahifadhi Misikiti ambamo Waislamu huitwa
kwa ajili ya Swala, mara tano kwa siku, kila siku.

Haifikiriki kwa Muislam yohyote kuvuruga kwa namna yoyote (achilia mbali shambulio
la mabomu) sehemu takatifu yenye taadhima kama hiyo ambapo Waislam hukusanyika kwa
ajili ya Ibada ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, Muumba wa Ulimwengu.

Haram hii ya Samarrah inayohifadhi Kuba ya wawili kati ya hawa watu mashuhuri katika
historia ya Uislamu pia ni sehemu yenye umuhimu mkubwa wa kihistoria. Kwani, ndani
ya eneo la Haram Tukufu hiyo, ni sehemu ya "ghaiba" (aliyochukuliwa na Allah,
kuwekwa mfichoni mwaka 260 Hijiria) ya Imam Mahdi, mtoto wa Imam Hasan al-Askari.
AL-MAHDI (kwa mujibu wa itikadi ya kiislamu) atajitokeza hapo baadae kuujaza
ulimwengu na haki kwani utakuwa umejaa ukandamizaji na dhulma.

Jumuiya ya Shia ya Tanzania inalaani vitendo vya kiwoga vya namna hiyo,
vilivyochochewa kutokana na tamaa ya madaraka kutoka kwa mtu yeyote, au kundi lolote
au mataifa yoyote.

Kwa ajili ya kuomboleza, Jumuiya ya Shia ya Tanzania imeitisha kipindi cha siku 7 za
maombolezo kuanzia tarehe 23 Feb. 2006.

Jumuiya ya Khoja Shia Ithnaashari Jamat ya Dar-es-Salaam

   
   Vitabu vya Kiarabu
» Orodha ya bei ya Vitabu vya Kiarabu
 
 
  Copyright © Alitrah, 2003. All rights reserved