| ABU
HURAIRAH
YALIYOMO
» Abu Hurairah Na Hadith
» Idadi
» Kukiri
» Asili
Ya Abu Hurairah
» Hali
Yake Kiakili Na Kimwili
» Kuhadithia
Hadith Nyingi Mno
» Abu
Hurairah Kupata Fahamu Ya Ajabu
Abu
Hurairah Na Hadith ?
Kila kitu, baadaye kilikuja kupitia yeye.
Baadhi ya sheria na itikadi za Dini, yote
hayo yalikuja kupitia sentenso zake ambazo
hazikuwa katika dini asili hapo mwanzoni.
Je ni sentenso ngapi unazozidhania wewe
kuwa ziliwatenganisha Wakristo kuacha uasili
wao ?
Yupo mtu
mmoja aitwaye ABU HURAIRAH ambaye historia
yake mimi nitaweleteeni hapo mbele baada
ya punde. Mtu huyu anasema mwenyewe :
Amehadithia
Abu Hurairah:
Hakuna Sahaba hata mmoja wa Mtume Muhammad
Mustafa s.a.w.w. kama mimi ambaye amehadithia
Hadith zaidi yangu isipokuwa 'Abdallah bin
Amr (bin al-'As) ambaye alikuwa akiziandika
ambapo mimi sikufanya hivyo.
Juzuu zote
tisa za Sahih Bukhari zina Ahadith 7,068.
Kati ya hizo kiasi cha Ahadith 1100 zimenakiliwa
na mtu huyu, yaani tuseme katika maneno
mengine kuwa yeye amenakili Ahadith kiasi
cha 15.56% za Ahadith zote za Sahih Bukhari
(kiasi cha 1/6).
(Hapa mbeleni
nitawapatieni idadi sahihi za Ahadith alizozinakili
Abu Hurairah katika Sahih Muslim).
Kama vile
nilivyoonyesha juu ya "Abu Hurairah",
yeye alijipinga mwenyewe na vile vile kisayansi.
Hadith ifuatayo ni wazi ambapo yeye anainakili
kwani inapingana na vile ‘Aisha bint
Abu Bakr ibn Abu Quhafa na ‘Umm Salamah
walivyoipokea. Iwapo sisi tutakubali kuwa
‘Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa
na ‘Umm Salamah walikuwa katika nyumba
ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. wakati
mwingi zaidi kuliko wake zake wengine, basi
kwa urahisi tutambua pale penye tatizo.
Haya yapo
katika ukurasa wa 81, katika sura:
Iwapo mtu aliye katika hali ya saumu akiamka
asubuhi akiwa katika Janaba (je saumu yake
itakuwa sahihi ?)
Hadith
hii imetarjumiwa na mtarjumu tu hadi mwishoni
mwa aya ya kwanza. Kufikia hapo, aliacha
kutarjumu. Hata hivyo, bado ipo katika lugha
ya Kiarabu. Kiasi kinachobakia ni tarjuma
yangu. Iwapo wewe hautataka kuniamini, ninakushauri
urejee katika maandishi ya Kiarabu. Zaid
ya hayo, mimi nitakuletea vianzio zaidi
kwa ajili ya kuelezea na tarjuma nilioyoifanya.
Amehadithia
‘Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa
na Umm Salamah:
“Baadhi za nyakati Mtume Muhammad
Mustafa s.a.w.w. alikuwa akiamka asubuhi
huku akiwa katika hali ya janaba baada ya
kujamiiana na wake zake. Yeye alikuwa akioga
na kufunga saumu.
Imehadithiwa
na Abu Bakr bin 'Abdur-Rahman : Mimi na
baba yangu tulimwendea'Aisha naye akasema
:
"Mimi ninatoa shuhuda kuwa Mtume Muhammad
Mustafa s.a.w.w. nyakati zingine alikuwa
akiamka asubuhi akiwa katika hali ya Janaba
kwa sababu ya kujamiiana, na wala si kutokwa
manii usingizini na alikuwa akifunga saumu
siku hiyo.” Kutoka hapo alimwendea
Umm Salamah ambaye nae pia alihadithia hivyo
hivyo.
Marwan
alimwambia Abdu-Rahman ibn Harith: Kula
kiapo kwa kuyasikia haya, Abu Hurairah atapiga
makelele. Wakati huu, Marwan alikuwa mjini
Madinah.
Abu Bakr
akasema: Abd-Rahman hakupendezewa na haya.
Baadaye ikatokezea kuwa tukakutana Dhi-Hulaifah
ambapo Abu Hurairah alikuwa na kipande cha
ardhi.
Abd-ar-Rahman
akamwambia Abu Hurairah:
Mimi nakwambia haya, na iwapo Marwan asingelikuwa
ameniuliza mimi ( kwa kula kiapo) haya,
basi mimi nisingelizungumzia hayo kwako
wewe. Ndipo hapo alipoitaja Hadith hiyo
aliyoelezwa na ‘Aisha bint Abu Bakr
ibn Abu Quhafa na Umm Salamah. Yeye (Abu
Hurairah) alisema: al-fadhl Ibn Abbas ameninakili
mimi hivyo yeye ni mtu aliye elimika zaidi.
Hammam na Ibn Abdullah Ibn Umar wamenakili
kutokea Abu Hurairah kuwa Mtume Muhammad
Mustafa s.a.w.w. aliamrisha kufunguliwa
kwa saumu (na msifunge), (ni dahiri) kuwa
mapokezi ya mnyororo huo (ni kutokea ‘Aisha
bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa na Umm Salamah
) unaaminiwa zaidi.
Swali :
Abu-Hurairah (RA) alikuwa karibu mno na
Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kwa miaka
michache, hata hakwenda sokoni.
Jibu :
Je unaelewa ni kwa kipindi gani Abu-Hurairah
alikuwa pamoja na Mtume Muhammad Mustafa
s.a.w.w.?
Jibu la
swali linapatikana kutokea marejeo ya Ki-sunni:
1. al-Milala wa al-Nihal, ya ibn al-Jawzi,
Pub. Egypt.
2. Sirat Ibn Hisham, Pub. Egypt.
Abu-Hurairah
alisimu miaka miwili tu kabla ya kifo cha
Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.
Hivyo,
itawezekanaje kwake yeye kuripoti Ahadith
2000 katika Sahih al-Bukhari peke yake,
wakati ambapo zipo Ahadith chache kabisa
zilizoripotiwa na Al-Imam ‘Ali ibn
Abi Talib a.s., Al-Imam Hassan ibn ‘Ali
ibn Abi Talib a.s., Al-Imam Hussain ibn
‘Ali ibn Abi Talib a.s. au Bi.Fatimah
az-Zahra a.s. Je utaelezaje masuala kama
haya? Mimi kwa hakika ninapendelea katika
malengo na majibu yako ya kisayansi huku
ukisaidiwa na baadhi ya marejeo.
Jibu :
1) Abu Hurairah alikuwa pamoja na Mtume
Muhammad Mustafa s.a.w.w. kwa muda wa masaa
24 !!! Na hivyo ndivyo alivyoweza kuzielezea
Ahadith zaidi ….
2) Yeye alizielezea Ahadith nyingi mno kwa
sababu ya kuwa pamoja na Masahaba wengineo
…. Kwa hakika Masahaba walikuwa ni
Waislamu wema na waliokuwa wakiaminiana,
na hivyo ndivyo alivyoweza kuzichukua baadhi
ya ahadith kutokea Masahaba ….
Jibu:
Ama kwa kuhusiana na upinganashi unaotolewa,
kile niwezacho kukisema mimi ni kwamba inambidi
msomaji arejee vitabu vya Fiq-h!!!! Na haya
nimeyasema kwa mara nyingi zilizopita …..
kwani kwa kuutolea uamuzi Hadith, inakubidi
urejee vitabu vya Fiq-h …. Kwani si
jambo la moja kwa moja. Mfano wa kitabu
cha Fiq-h al-Sunnah.
Kwa upande
wa pili, iwapo wewe utakuwa na kitabu cha
Fiq-h al-Sunnah naomba uzingatie kuwa wakati
Said Sabiq (mmoja wa Wanazuoni wa Kisunni
anayeheshimiwa na vile vile mwandishi wa
vitabu vinavyotambulikana kama kitabu tulichokitaja
hapo juu ) anapozungumzia baadhi ya masuala,
mara nyingine yeye huzungumzia kimtazamo
wa Kishi’a kwa suala hilo. Kwa mfano:
Zawaj al-Mut’ah, Qanun al-Hawal al-Shakhsiyyah
(Kanuni za Ndoa). Vile vile chunguza mwelekeo
wake pale anapowazungumzia Waislamu Mashi’a
au Wanazuoni wa Ki-Shi’a!
Tafadhali
sana naomba unijulishe kile unachokifikiria
baada ya kupitia Sura mbili za kitabu hicho.
Idadi
Miongoni mwa Masahaba wote na wale waliokuwa
wamemtembelea Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.,
ni wachache tu ambao walioziripoti Ahadith
katika Sahih . Idadi yao ni ndogo kabisa
hata kuliko idadi ya vidole. Wakati ambapo
riwaya nyingine inasemwa kuwa kiasi cha
watu 1400 walikwenda pamoja na Mtume Muhammad
Mustafa s.a.w.w. huko Hudaibiyyah. Mji mtukufu
wa Madina ulikuwa na wakazi zaidi ya 3000.
Katika Vita vya Makkah (Fath-al-Mubin),
zaidi ya watu 10,000 walishiriki. Katika
Hajj ya mwisho ya Mtume Muhammad Mustafa
s.a.w.w. , kiasi cha watu idadi hiyo walikuwa
pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.
Kutokea watu wote hawa, ni watu wachache
mno waliotajwa katika Sahih. Miongoni mwa
hao waliotajwa wapo watu kama Abu Hurairah
ambaye alisimu kiasi cha miaka mitatu tu
kabla ya kifo cha Mtume Muhammad Mustafa
s.a.w.w. Mtu mwingine ni ‘Aisha bint
Abu Bakr ibn Abu Quhafa ambaye nae pia amenakiliwa
Ahadith nyingi. Tuangalie alikuwa na umri
gani :
Amehadithia
babake Hisham:
Bi.Khadija alifariki miaka mitatu kabla
ya Hijrah ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.
kwenda Madina. Na huko Mtume Muhammad Mustafa
s.a.w.w. aliishi kwa muda wa miaka miwili
au zaidi na ndipo hapo alipomwoa ‘Aisha
bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa aliyekuwa na
umri wa miaka sita, na ndoa hiyo ilitimika
pale alipokuwa na umri wa miaka tisa.
Mahisabu
ya kirahisi yanasema:
1)- Mtume
Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimposa ‘Aisha
bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa kabla ya Hijra
ya kwenda Madina (mwaka mmoja kabla ya Hijra).
Wakati huo ‘Aisha bint Abu Bakr ibn
Abu Quhafa alikuwa na umri wa miaka sita.
(Riwaya
nyingineyo inasema kuwa ‘Aisha bint
Abu Bakr ibn Abu Quhafa mwenyewe anasema
kuwa yeye alikuwa bado akicheza na michezo
ya kitoto katika siku hizo).
2)- Mtume
Muhammad Mustafa s.a.w.w. almwoa ‘Aisha
bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa katika mwaka
wa pili wa Hijra, pale ‘Aisha bint
Abu Bakr ibn Abu Quhafa alipokuwa na umri
wa miaka tisa.
3)- Tukuchukulia
kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliishi
kwa miaka 10 baada ya Hijrah, ‘Aisha
bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa aliishi kwa
muda wa miaka 8 tu ya utu uzima wake pamoja
na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.
Jambo moja
napenda kuongezea hapa, nitatoa marejeo
halisi, kuwa wanawake huwa ni watu wepesi
kusahau maneno halisi au hata maneno yenyewe.
Kwa hakika haya ni maumbile ya wanawake.
Na hivyo kwa kuwa ‘Aisha bint Abu
Bakr ibn Abu Quhafa alikuwa ni mwanamke
hivyo ni jambo la kawaida kutegemea kuwa
yeye pia atakuwa amesahau baadhi ya Ahadith
katika hali ya uhalisi wake.
Sasa naomba
tuchunguze idadi ambazo mimi ninawaleteeni
mbele yenu kuhusiana na watu mbalimbali
waliozipokea ahadith. Mimi sidai kuwa idadi
hiyo ni sahihi kabisa, kwani mimi mwenyewe
sikuzihisabu kwa vidole.
Ama kwa
uhakika mimi binafsi nimezihisabu Ahadith
zilizopokelewa na Al-Imam ‘Ali ibn
Abi Talib a.s. na wana wake.
Baadhi
ya ahadith ambazo zimeandikwa na Imam Bukhari
kwa kurejewa vile vile zimeingizwa katika
idadi hiyo.
Kimatokeo,
itakubidi baadhi ya nyakati upunguze kwa
100 kutokea humo.
Jumla ya
Ahadith zilizopo katika Juzuu 9 za Bukhari:
7,068
| Na. |
JINA |
IDADI |
% |
| 1 |
Aisha
bint Abu Bakr |
1250
|
17.68 |
| 2 |
Abu
Hurairah |
1100
|
15.56 |
| 3 |
Ibn-Umar,
mwana wa Umar |
1100 |
15.56 |
| 4 |
Anas-Ibn-Malik |
900 |
12.73 |
| 5 |
Abdullah-Ibn-Abbas |
700
|
9.9 |
| 6 |
Jobair-Ibn-Abdullah |
275 |
3.89 |
| 7 |
Abu-Musa-Ashari |
165
|
2.33 |
| 8 |
Abu-Said-Al-Khudhri |
130 |
1.84 |
| 9 |
Ali
ibn Abi Talib |
79 |
1.11 |
| 10 |
Umar-Ibn-Khattab |
50 |
0.71 |
| 11 |
Umm
Salamah |
48 |
0.68 |
| 12
|
Abdullah-Ibn-Masud |
45 |
0.64 |
| 13 |
Muawiyah
Ibn-Abu Sufian |
10 |
0.14 |
| 14 |
Hassan
ibn Ali ibn Abi Talib |
8 |
0.11 |
| 15 |
Hussain
ibn Ali ibn Abi Talib |
2 |
0.03 |
| 16 |
Ali-Ibn-Husain |
6 |
0.08 |
| |
JUMLA |
|
83 |
|
Kama vile
uonavyo wewe mwenyewe katika jedwali la
hapo juu, zimechukuliwa Ahadith chache kabisa
zilizopokelewa na Al-Imam ‘Ali ibn
Abi Talib a.s. na Watoto (Wajukuu wa Mtume
Muhammad Mustafa s.a.w.w. ) wake. Mimi sijawapatieni
bado majina ya wengine waliozielezea Ahadith.
Mwandishi wa kitabu hiki cha Bukhari alikuwa
akiishi katika zama za Al-Imam Muhammad
al-Baqir a.s., mwana wa Al-Imam Zainul ‘Abidiin
a.s. na vile vile zama za Al-Imam Ja’afar
as-Sadiq a.s. Kwa hakika yeye hakutaja hata
Hadith moja kutokea hao. Kwa hakika hiki
ndicho kilikuwa ni kipindi ambacho Al-Imam
Muhammad al-Baqir a.s. na Al-Imam Ja’afar
as-Sadiq a.s. walikuwa wakizielezea Ahadith
zilizowafikia wao kutokea Wazazi (a.s.)
wao hadi Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib
a.s. na, mwisho ambapo ndipo kutokea kwa
Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. mwenyewe.
Katika maneno mengine, Imam Bukhari hakuwathamini
hawa Watoto wa Al-Imam ‘Ali ibn Abi
Talib a.s. iwapo walistahili kuzielezea
Ahadith, na aliwadhania wao kuwa ni waongo.
Kwa hakika
ukipitia vianzio vya Kishi’a, utaona
kuwa watu hawa hawakuwa kimya bali walikuwa
ni waelezaji wakubwa wa Ahadith za Mtume
Muhammad Mustafa s.a.w.w. kutokea Wazazi
a.s. wao hadi kufikia Al-Imam ‘Ali
ibn Abi Talib a.s. na Mtume Muhammad Mustafa
s.a.w.w. mwenyewe. Je jambo hili si la kuvutia
?
Kukiri
?
Hadithi ifuatayo si ngeni vile yaliyopo
ndani mwa Hadith yanavyo kwenda. Mwanzani
Abu Hurairah ananakili Hadith kutokea Mtume
Muhammad Mustafa s.a.w.w. Na pale watu walipomwuliza
iwapo yeye Abu Hurairah aliisikia mwenyewe
hadith hiyo kutokea kwa Mtume Muhammad Mustafa
s.a.w.w. au sivyo, yeye alijibu kuwa yeye
hakumsikia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.
na akaielezea yeye mwenyewe.
1)- Kile
nikuombacho wewe unisaidie kuigawa hadith
hiyo ya kwanza katika sehemu mbili :
a)- Sehemu ya kwanza iwe ile ambayo imesemwa
na
Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.
b)- Sehemu ile ambayo imesemwa na Abu Hurairah
tu.
2)- Nitakuomba
unieleze kwa uwazi kabisa ni kwa nini watu
walimwuliza iwapo maneno hayo yalikuwa yametamkwa
na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Hadi
pale kiwango cha elimu yangu inapohusika,
watu waliuliza hivyo pale walipoisikia Hadith
ikiwa ngeni kwao, kama vile Hadith zinazozungumzia
mambo ya maishani na baadhi ya matukio ambayo
yalikuwa hayaaminiki kwao, na ambayo kwa
hakika yanatokezea nyakati hizi. Je ni jambo
gani la kustaajabisha katika Hadith hii,
na ni kwa nini watu walimwuliza Abu Hurairah
iwapo alikuwa akizungumza kile alichokisikia
kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.
au sivyo.
3)- Nitapendelea iwapo wewe kwa uwazi utaniambia
kile ambacho kisingelitokea iwapo watu wasingelimwuliza
Abu Hurairah iwapo sehemu yoyote ile ya
hadith ilikuwa kwa hakika imezungumzwa na
Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. au sivyo.
4)- Iwapo
watu wasingelimwuliza Abu Hurairah iwapo
Hadith hiyo ilikuwa imezungumwa na Mtume
Muhammad Mustafa s.a.w.w. au sivyo, kidhahiri,
watu wangeliichukulia Hadith nzima kama
ni maneno aliyoyasema Mtume Muhammad Mustafa
s.a.w.w. Ukweli ni kwamba, vyovyote vile,
Abu Hurairah amesema baadhi ya maneno yake
mwenyewe na kuongezea baadhi ya maneno katika
Hadith ambapo (inawezekana) imetamkwa na
Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Mimi nitapenda
uniambie ni kwa nini unamwamini mtu kama
huyo ambaye anaongezea baadhi ya maneno
yake mwenyewe katika maneno ya Mtume Muhammad
Mustafa s.a.w.w.
5)- Je
unaweza kuniorodheshea Hadith zote ambazo
zimeelezwa na Abu Hurairah na kwamba zimekubaliwa
na Imam Bukhari na Muslim, na kuchora mstari
ulio wazi kabisa baina ya maneno yaliyozungumzwa
na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. au Abu
Hurairah mwenyewe.
Kwa hakika
mimi sielewei vile mtu anavyojiruhusu mwenyewe
kuzungumza kile ambacho hajakisikia kutokea
Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na hata
akathubutu kuziingiza katika maneno ya Mtume
Muhammad Mustafa s.a.w.w. hata bila ya kutoa
tahadhari. Au ni kwa nini anazungumzia vya
kwake mwenyewe kabla ya kuelezea wazi wazi
hapo mwanzoni mwa maneno yake kuwa hayo
yalikuwa ni maneno yake binafsi na kamwe
si ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.?
Mfano wa
pili unaonyesha wazi wazi kuwa Abu Hurairah
ameongezea (inawezekana) katika yale aliyoyazungumza
Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Je itakuwaje
pale ambapo hakuna mtu yeyote aliyetutanabahisha
kuhusu kuongezewa maneno ya ziada ya Abu
Hurairah ?
Amehadithia
Abu Hurairah kuwa Mtume Muhammad Mustafa
s.a.w.w. amesema:
"Sadaqa iliyo bora kabisa ni ile ambayo
itolewayo wakati mtu awapo tajiri, na mkono
utoao ni bora kuliko mkono ule unaopokea,
na wewe inakubidi uanze kuwasaidia kwanza
wale wanaokutegemea.’ Mke husema,
‘Wewe ama unipatie chakula au talaqa.’
Mtumwa husema, ‘Nipe chakula na ufaidi
huduma zangu.’ Mtoto husema, ‘Nipe
chakula, je unaniachia kwa nani?’
Watu wakasema, ‘Ewe Abu Hurairah!
Je hayo umeyasikia kwa Mtume Muhammad Mustafa
s.a.w.w. ?’ Naye akajibu, ‘La,
bali hayo ni kutokana mimi mwenyewe.”
Nitapenda
kujua ni kwa nini Abu Hurairah alizoea kuongezea
mahala penginepo pia ?
Anas bin
Malik amesema kuwa Mtume Muhammad Mustafa
s.a.w.w. amesema:
“Msifanye vinywaji katika Ad-Dubba'
wala katika al-Muzaffat. Abu Hurairah alizoea
kuongezea zaidi maneno al-Hantam na An-Naqir.
Imehadithiwa na Abu Hurairah kuwa mtu mmoja
alimwijia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.
na kusema :
“Mimi nilijamiiana na mke wangu katika
siku ya Mwezi wa Ramadhani (akiwa katika
saumu).”
Mtume Muhammad
Mustafa s.a.w.w. alimwuliza:”Je unaweza
kumfanya mtumwa mmoja awe huru?”
Mtu huyo
akajibu kuwa hawezi. Ndipo hapo tena Mtume
Muhammad Mustafa s.a.w.w. alipomwuliza:”Je
unaweza kufunga saumu kwa muda wa miezi
miwili mfululizo ?”
Tena mtu
huyo akajibu kuwa asingeweza. Basi Mtume
Muhammad Mustafa s.a.w.w. akamwuliza: “Je
unaweza kuwalisha masikini 60 ?”
Hapa tena
mtu huyo akajibu kuwa asingeliweza kuwalisha
masikini sitini.
(ABU HURAIRAH
AKAONGEZEA):
Ndipo hapo kikapu kilichokuwa kimejaa tende
kilipoletwa mbele ya Mtume Muhammad Mustafa
s.a.w.w. na akamwambia mtu huyo, “Walishe
(masikini) kwa haya kama kaffarah.”
Mtu huyo
akasema, (Je niwalishe haya) masikini kuliko
sisi wenyewe? Hakuna nyumba ya wa masikini
kuliko sisi baina ya milima ya Mji wa Madina.”
Kwa hayo
Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akasema,
“Basi walishe watu wa nyumba yako
kwa hayo.”
Asili
Ya Abu Hurairah
Masunni kwa kawaida huzitaja baadhi ya Ayah
za Qur’an Tukufu kuonyesha kuwa Masahaba
ambao walishiriki katika Viapo vya Hudaibiyyah
wanalo daraja la juu (mema) na wanaheshimiwa
mno. Vyema, hapa, mimi sitaki kujiingiza
katika usahihi wa kuitafsiri na kuielewa
kwake.
Je wewe
unajua kuwa wakati huo Abu Hurairah hakuwa
Mwislamu, na wala hakuwa miongoni mwa wale
walioshuhudia Viapo vya Hudaibiyyah ? Naam
! Abu Hurairah kamwe hakushuhudia Viapo
vya Hudaibiyyah !
Abu Hurairah
alikuwa Myahudi, na alisimu Siku ya Khaibar
ambayo ilikuwapo mwaka mmoja baada ya Viapo
vya Hudaibiyyah, na aliishi miaka mitatu
tu pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.
1)- Abu Hurairah alisilimu siku ya Khaibar.
Haya yanathibitishwa na Jabir ibn ‘Abdullah
(Hadith ya pili).
Abu Hurairah alimwijia Mtume Muhammad Mustafa
s.a.w.w. katika siku ya Khaibar
Mimi sihitajiki
kusisitiza suala hili kuwa Vita vya Khaibar
vilikuwa baina ya Waislamu na Mayahudi.
Abu Hurairah alikuwa Myahudi kabla ya kusilimu.
2)- Abu
Hurairah alikuwa pamoja na Mtume Muhammad
Mustafa s.a.w.w. kwa kipindi cha miaka mitatu
tu (yeye mwenyewe anathibitisha hayo katika
Hadith ya kwanza)
“Nilikuwa pamoja na Mtume Muhammad
Mustafa s.a.w.w. kwa kipindi cha miaka mitatu”3)-
Labda, wewe unaelewa vyema vile wengineo
walivyomsalimia pale aliposilimu siku hiyo.
Amehadithia
Abu Hurairah:
Mimi nilikuwa pamoja na Mtume Muhammad Mustafa
s.a.w.w. kwa muda wa miaka mitatu, na katika
miaka iliyokuwa imebakia katika umri wangu
nilikuwa na shauku kubwa ya kuzielewa ahadith
za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kama
vile nilivyokuwa katika miaka mitatu ile.
Mimi nimemsikia akisema, akionyesha kwa
mikono yake hivi, : ‘Kabla ya Saa,
utapigana na watu ambao watakuwa na viatu
vya manyoa na wakiishi al-Bariz.’
(Sufiani, mnakili wa mnakili, alisema mara
moja, “Na hao ndio watu wa al-Bazir.”
Amehadithia
Ja’bir bin 'Abdullah:
“Kuwa yeye alipigana katika Ghazwa
kuelekea Najd pamoja na Mtume Muhammad Mustafa
s.a.w.w. na wakati Mtume Muhammad Mustafa
s.a.w.w. aliporejea , naye pia, alirejea
nae. Wakati wa usingizi wa mchana uliwachukua
wakati walipokuwa katika bonde lililokuwa
limejaa miti ya miiba. Mtume Muhammad Mustafa
s.a.w.w. aliteremka chini ya farasi wake
na hivyo ndivyo walivyokuwa watu wote wakatawanyika
katikati ya miti hiyo ya miiba, wakijistiri
katika vivuli vya miti hiyo. Mtume Muhammad
Mustafa s.a.w.w. alijipatia kivuli chini
ya mti wa Samura na kuuning’iniza
upanga wake juu ya mti huo. Sisi tulilala
kidogo ambapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.
alituita kwa ghafla, na tulipomwendea tukakuta
kuwa Mbedui mmoja alikuwa ameketi pamoja
nae. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akasema
kuwa Mbedui huyo aliuchukua upanga wake
kutokea ala yake wakati yeye akiwa amelala.
Wakati nilipoamka, nikaukuta upanga huo
upo mkononi mwake na akiniambia “Je
ni nani anayeweza kukuokoa kwangu?”
Mimi nikamjibu, “Allah swt”
Na sasa huyu hapa ameketi.” Mtume
Muhammad Mustafa s.a.w.w. hakumwadhibu (kwa
hayo).
Kwa kupitia kundi lingine la waelezaji wengine
wa riwaya, Ja’bir alisema :
“Sisi tulikua pamoja na Mtume Muhammad
Mustafa s.a.w.w. (katika Vita vya) Dhat-ul-Riqa’,
na tulitokezea chini ya mti wenye kivuli
na tukamwachia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.
(apumzike chini ya kivuli chake). Alitokezea
Mapagani mmoja huku upanga wa Mtume Muhammad
Mustafa s.a.w.w. ulipokuwa ukining’inia
mtini. Mpagani huyo aliutoa upanga huo kutokea
ala yake kwa kisiri na alimwambia Mtume
Muhammad Mustafa s.a.w.w. ‘Je waniogopa
mimi?’ Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa
s.a.w.w. alimjibu, ‘hapana.’
Ndipo hapo Mpagani huyo aliposema,’Je
ni nani anayeweza kukuokoa wewe kutoka kwangu?’
Kwa hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.
alimjibu, ‘Allah swt .’
Masahaba
wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. walimtishia
huyo, na mara Iqamah ya Sala ilisemwa, na
Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alisali
raka’a mbili za Sala ya Khofu pamoja
na kundi mojawapo ya makundi mawili, na
kundi hilo lilikwenda pembeni, na hapo tena
Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alisali
Raka’a mbili zinginezo pamoja na kundi
lingine. Hivyo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.
alisali jumla ya Raka’a nne ambapo
watu walisali raka’a mbili tu.”
(Mwelezaji
wa mwelezaji) Abu Bishr aliongezea,
Mtu huyo alikuwa Ghaurath bin al-Harith
na Vita vilipiganwa dhidi ya Muharib Khasafa."
Jabir akaongezea, "Sisi tulikuwa pamoja
na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. hapo
Nakhl ambapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.
alisali Sala ya Khofu." Abu Hurairah
akasema, "Mimi nilisali sala ya Khofu
pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.
wakati wa Ghazwa (yaani Vita) vya Najd.”
Abu Hurairah
alimwijia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.
siku ya Khaibar !!
Amehadithia
'Anbasa bin Said:
Abu Hurairah alimwijia Mtume Muhammad Mustafa
s.a.w.w. na kumwuliza (kutaka hisa katika
mali iliyopatikana katika Vita vya Khaibar
au ngawira ). Kwa hayo, mmoja wa wana wa
Said bin al-'As alimwambia Mtume Muhammad
Mustafa s.a.w.w. ‘Ewe Mtume wa Allah
swt ! Usimpe huyo (Abu Hurairah ).’
Kwa hayo Abu Hurairah alimwambia Mtume Muhammad
Mustafa s.a.w.w. ‘Huyu ndiye mwuaji
wa Ibn Qauqal.’ Mwana wa Sa’id
akasema, ‘Maajabu gani ! Jitu dogo
(au mwovu) litokalo Qadum Ad-Dan!"
Amehadithia
Abu Hurairah : Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.
alimtuma Aban kutokea Madina kwenda Najd
akiwa Kamanda wa Sariya. Aban na wenzake
walimwijia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.
huko Khaibar baada ya Mtume Muhammad Mustafa
s.a.w.w. akiwa ameishaikomboa Khaibar, na
mafigo ya farasi zao zilitengenezwa kwa
moto wa mitende. Mimi nilisema, ‘Ewe
Mtume wa Allah swt ! Usiwape hisa ya Ngawira.’
Kwa hayo Aban akasema ( kuniambia mimi),
“Maajabu ! Wewe unashauri jambo ingawaje
wewe ni wewe, ewe mtu mdogo (au mwovu) utokeae
Ad-Dal (myungiyungi)!” Kwa kuyasikia
hayo, Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akasema,
“Ewe Aban, kaa chini!” Na hakuwapa
hisa yoyote.
Amehadithia
Said:
Aban bin Said alimwijia Mtume Muhammad Mustafa
s.a.w.w. na kumsalimia. Abu Hurairah akasema,
Ewe Mtume wa Allah swt ! Huyu (Aban) ni
mwuaji wa Ibn Qauqal." (Kwa kuyasikia
hayo), Aban alimwambia Abu Hurairah, "Usemayo
wewe yanavyostaajabisha! Ewe, mtu mdogo
( au mwovu) ukitokea Qadum Dan, ukinituhumu
mimi kwa (mauaji) ya mtu ambaye Allah swt
amemjaalia (shahada) kwa mikono yangu, na
kwamba Allah swt ameharamisha udhalilisho
wangu mikononi mwake.’
Hali
Yake Kiakili Na Kimwili
1)- Baada ya Abu Hurairah kusilimu, alikuwa
hana kitu chochote. Yeye alikuwa akiwaambia
watu wasome Ayah ya Qur’an Tukufu,
si kwamba alikuwa akitaka kufaidika nayo.
Yeye alikuwa akitaka mtu huyo awe na hisia
ya kidini na hivyo aweze kumwalika Abu Hurairah
kwa ajili ya chakula cha mchana au usiku.
Suala hili linajulika vyema kabisa kama
“Kuchanganya Tumbo na Dini.”
( Au kuchanganya Dini na pesa, tumbo, uwezo,…
au kwa vitu vya kawaida , au visivyo na
maana).
2)- Hata
watu hawaamini kuwa Abu Hurairah anaweza
kuhadithia hadith kiasi hicho. ( Hakuna
marejeo sasa : Imesemwa kuwa Abu Hurairah
amehadithia Hadithi 40,000 katika uhai wake.
Tukigawa Hadith hizo kwa kipindi cha miaka
mitatu ya Usahaba wake, tunapata Hadith
36 kwa siku (!!! ).
Marejeo
niliyokwishayatoa hapo nyuma zinathibitisha
kuwa, yeye mwenyewe Abu Hurairah, amekiri
kuwa hakuna mtu yeyote miongoni mwa Masahaba
ambaye amehadithia Hadith nyingi kama za
kwake. Tukitambua ukweli huu kuwa yeye ndiye
mtu wa pili katika kiwango cha kuhadithia
wingi wa Ahadith katika Bukhari na Muslim,
basi tunafikia uamuzi kuwa yeye Abu Hurairah
atakuwa amehadithia Hadith nyingi mno zaidi
ya hizo ambazo zimerekodiwa katika vitabu
hivi viwili.
Katika
mojawapo ya Hadith, yeye Abu Hurairah mwenyewe,
amekiri kuwa watu walikuwa wakimtuhumu yeye
kwa ukichaa au mwenda wazimu.
3)- Jambo
la kuvutia hapa ni kwamba hakuna hata Hadith
moja iliyohadithiwa na mtu yeyote mwingine
(mbali na yeye Abu Hurairah mwenyewe) kuzungumzia
mema ya Abu Hurairah. Iwapo wewe utachunguza
Bukhari na Muslim nzima kuhusu sifa ya Abu
Hurairah, basi Hadith yoyote ile utakayoipata
kuhusiana na Usahaba wake pamoja na Mtume
Muhammad Mustafa s.a.w.w., na elimu yake
basi itakuwa imehadithiwa na yeye mwenyewe
(Abu Hurairah mwenyewe na wala si mtu mwingine)!
Ambapo upande mwingine, wewe utakaposoma
wema na sifa za Al-Imam ‘Ali ibn Abi
Talib a.s. ( na wengineo kama Salman, Umar,
Zubair, ….), basi utaona kuwa wapo
wengine wanaomsifu Al-Imam ‘Ali ibn
Abi Talib a.s. (na wengineo) kwa Hadith
mbalimbali. Lakini haya vyovyote vile hayapatikani
pamoja na Abu Hurairah. Hadith zote kama
: Mimi nilikuwa mtoto mzuri, au nilifanya
hivi na vile zimehadithiwa na Abu Hurairah
mwenyewe tu (na wala si mtu mwingine).
Mimi nakutaka
unijibu iwapo utakubaliwa ushahidi wa mtu
ajisemaye kuwa yeye ni mtoto mwema.
Amehadithia
Abu Hurairah:
“Watu walikuwa na desturi ya kusema
kuwa Abu Hurairah anahadithia Hadith nyingi
mno.”
Kwa hakika
mimi daima nilijiweka karibu mno na Mtume
Muhammad Mustafa s.a.w.w. na nilikuwa nikiridhika
kwa kile kilichoshibisha tumbo langu. Mimi
sikula mkate uliochachuka na wala sikuvaa
mavazi yalirembeshwa kwa mistari, na kamwe
hakuna mwanamme au mwanamke aliyekuwa amenihudumia
mimi, na mara nyingi nilikuwa nikilibana
tumbo langu kwa mawe kwa sababu za njaa,
na mimi nilikuwa nikiwaambia watu wanisomee
Ayah ya Qur’an Tukufu ingawaje nilikuwa
nikiijua, ili kwamba anichukue nyumbani
kwake na kunilisha chakula. Kwa hakika miongoni
mwa watu waliokuwa wakarimu kwa masikini
kuliko wote alikuwa ni Ja'far bin Abi Talib.
Kwa hakika yeye alikuwa akituchukua nyumbani
kwake na kutulisha chochote kile kilichokuwapo.
Yeye vile vile alikuwa akitupatia mifuko
(ya ngozi) tupu ya siagi ambayo alikuwa
akiichana na tukilamba chochote kile kilichokuwamo
ndani yake.”
Amehadithia
Abu Hurairah:
“Mimi niliambatana na Mtume Muhammad
Mustafa s.a.w.w. kwa ajili ya kulijaza tumbo
langu; na ndiyo kwa maana hiyo mimi sikula
mkate uliochomwa wala kuvaa nguo za hariri.
Na wala hakuna mtumwa kijakazi wala wa kiume
aliyenihudumia mimi, nami nilikuwa nikijifunga
mawe tumboni mwangu na nilikuwa nikimwomba
mtu yeyote anisomee Ayah ya Qur’an
Tukufu ingawaje nilikuwa nikiijua, ili kwamba
inawezekana akanichukua nyumbani kwake na
kunilisha chakula. Ja'far bin Abi Talib
alikuwa mkarimu kwa masikini, yeye alikuwa
akituchukua nyumbani kwake na kutulisha
chochote kile alichokuwanacho nyumbani mwake,
( na kama kulikuwa hakuna chochote kile),
yeye alikuwa akitupatia mifuko mitupu ya
ngozi ( ya asali au siagi) ambapo sisi tulikuwa
tukichana na kulamba chochote kilichokuwamo
kimebakia.”
Amehadithia
Muhammad:
Sisi tulikuwa pamoja na Abu Hurairah pale
alipokuwa akivaa nguo mbili za katani zilizokuwa
zimetiwa rangi ya udongo mwekundu. Yeye
alisafisha pua yake kwa nguo hiyo huku akisema,
‘Hongera ! Vyema sana ! Abu Hurairah
anasafisha pua yake kwa katani!
Ulifika
wakati ambapo mimi nilikuwa nikianguka bila
fahamu baina ya Mimbar ya Mtume Muhammad
Mustafa s.a.w.w. na nyumba ya ‘Aisha
bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa ambapo mtu
aliyekuwa akipita hapo alinikanyaga shingoni
kwa miguu yake, wakinichukulia mimi kuwa
mwenda wazimu (kichaa), lakina kwa hakika,
mimi sikuwa na ukichaa wowote, mimi sikuugua
chochote kile isipokuwa njaa tu.”
Amehadithia
Abu Hurairah:
Wakati mmoja ambapo nilipokuwa katika hali
ya ulegevu (kwa kutokana na njaa kali),
nilionana na 'Umar bin al-Khattab, hivyo
nilimwomba anisomee Ayah ya Qur’an
Tukufu. Yeye aliingia nyumbani mwake na
kunitafsiria. (Na mimi niliondoka zangu)
baada ya kutembea umbali kidogo, nilidondoka
chini juu ya uso wangu kwa sababu ya ulegevu
wangu ambao ulitokana na njaa kali mno.
Mara ghafla nikamkuta Mtume Muhammad Mustafa
s.a.w.w. akiwa amesimama kichwani mwangu.
Akaniambia, “Ewe Abu Hurairah!"
Nami nikamjibu, “Labbaik ewe Mtume
wa Allah swt na Siddiq!” kwa hayo
akanishika mkono, na kuniinua. Ndipo alipokuja
kujua kile kilichokuwa kikinisumbua. Hivyo
akanichukua nyumbani kwake na akaniagizia
bakuli kubwa la maziwa kwa ajili yangu.
Mimi niliyanywa maziwa hayo, na ndipo hapo
aliponiambia, “Kunya mengine, Ewe
Abu Hurairah !!” Hivyo, mimi niliyanywa
tena, kwa kumaliza, ambapo tena alisema,
“Kunya zaidi.” Hivyo mimi niliyanywa
tena hadi pale tumbo langu lilipojaa na
kuonekana kama bakuli. Baadaye mimi nilikutana
na ‘Umar na kumwelezea yote hayo yaliyotokea,
na kumwambia, “Mtu fulani, ambaye
anayestahiki zaidi yako wewe, alilichukua
suala hili. Kwa kiapo cha Allah swt, mimi
nilikwambia wewe unisomee Ayah ya Qur’an
Tukufu wakati ambapo mimi ninazielewa vyema
zaidi yako wewe.” Kwa hayo ‘Umar
aliniambia, “Kwa kiapo cha Allah swt!
Iwapo ningalikubali na kukushughulikia wewe,
basi ingalinipendezea kwangu mimi kuliko
kuwa na ngamia wazuri wekundu.”
Kujaaliwa
kwa ghafla uwezo maalum zaidi
Je hautaingiwa
na shaka iwapo mtu akijaaliwa kwa ghafla
uwezo maalum zaidi ya watu wengine, lakini
sisi hatujawahi kusikia kuwa Abu Hurairah
alikuwa na uwezo maalumu zaidi ya watu wengine.
Ghafla anatokezea mbele ya Mtume Muhammad
Mustafa s.a.w.w. na kuishi nae kwa muda
wa miaka mitatu na tunaona kuwa anakumbuka
kila kitu kwa nguvu fulani za kiajabu ?
Jambo hili
si la kumfanya mtu awe Msunni au Mshi’a
kwa kuulizia je Abu Hurairah alikuwa akiropoka
? Mtu huyu alikuwa akiutumia muda wake mdogo
huo pamoja na Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.
kwa kujipatia faida zake binafsi na kuendelea
kujipatia uhusiano kila pale palipojitokeza
jambo ambalo lilihitaji ushauri na maoni,
basi kwa nini yeye alijitokeza pamoja na
Hadith ambayo yeye kwa haraka kabisa aliikumbuka
kwa ukamilifu!!
Hususan
Abu Hurairah alikuwa akimchukia ‘Aisha
bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa na ni jambo
la kuzingatiwa kuwa yeye alitunga hadith
ambayo ‘Aisha bint Abu Bakr ibn Abu
Quhafa aliipinga wazi wazi kabisa.
Jambo la
kustaajabisha ni kwamba ubongo wa Abu Hurairah
uligeuka kuwa wa ajabu kabisa baada ya kifo
cha Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Jambo
lolote au suala lolote lililojitokeza wakati
wowote ule, basi yeye alizungumzia mambo
ambayo hakuna mtu mwingine aliyejua au kuyasikia
hapo kabla. Wow!
Kwa hakika
tunaona wazi kuwa mtu huyu alikuwa akijitakia
manufaa kwa ajili yake katika kujipatia
nafasi na harakati zake za kisiasa na kijamii.
Kuhadithia
Hadith Nyingi Mno ?
‘Aisha bint Abu Bakr ibn Abu Quhafa
amehadithia Hadith (1250) nyingi mno kuliko
Abu Hurairah katika Sahih Bukhari.
Ibn Umar
amehadithia (1100) kiasi kama cha Abu Hurairah
(1100) katika Bukhari. Idadi nimezitaja
hapo awali katika jedwali.
Mimi sikuulizia
ni kwa nini ‘Aisha bint Abu Bakr ibn
Abu Quhafa ameripoti hadith nyingi kiasi
hicho kutokea kwa Mtume Muhammad Mustafa
s.a.w.w. na wala sikuulizia kuhusu Ibn ‘umar,
au Ibn ‘Abbas au wengineo.
Lakini
nilichokiuliza ni: Itawezekanaje kwa mtu
aliyekuwa kasoro ya miaka mitatu aweze kuhadithia
Hadith nyingi kiasi hicho?
Tunayaachilia
mengineyo. Abu Hurairah amehadithia hadith
5,374 tu.
Iwapo tutachukua
kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alikuwa
miaka mitatu kamili pamoja na Abu Hurairah
:
5,374/3
= 1791.33 Ahadith kwa mwaka,
1791.33/(365-11)=
5.06 Ahadith kwa siku.
Wewe utaniuliza
kwa vipi tena ? Je itawezekanaje kwa mtu
kufanya hivyo kila siku ? Je kwa nini alikuwa
amejitolea kiasi hicho ambapo kulikuwapo
watu waliokuwa bora zaidi kuliko yeye, kama
vile ‘Umar, mtoto wake, Ibn ‘Abbas
na Abu Bakr hawakuweza kufanya hivyo ? (
Kwa uzani wa Abu Hurairah, hata Hadith 5
kwa siku ?) Bila ya kutaja kuwa Abu Hurairah
amehadithia Hadith zaidi mno kuliko Sahaba
yeyote, kutegemea kauli yake mwenyewe.
Baadhi
wanasema kuwa Abu Hurairah amehadithia kiasi
cha Hadith 40,000. Hata watu walikuwapo
karibu nae walishangazwa na mtu huyu kwa
kuhadithia kwake huku ( kwa kutegemea kauli
ya Abu Hurairah mwenyewe).
Sehemu
ya pili ni kwa nini mtu kama huyu amehadithia
sawa na riwaya za Agano la Kale ? ( sehemu
ambazo zimekanushwa na itikadi na imani
za Kiislamu ?)
Abu
Hurairah Kupata Fahamu Ya Ajabu?
Sasa ndipo wewe unaanza kuhisi nakisi ya
elimu yako. Je unajua kuwa Sahaba na Ndugu
wa Kijamaa wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.
Abdullah Ibn Abbas alipewa baraka za Mtume
Muhammad Mustafa s.a.w.w. na siku moja alimpiga
kwa mkono kifua chake na alimwomba Allah
swt akisema : “Allahumma faqqihhu
fiddini wa 'allimhu min ta'uwili l kitabi"
( Ewe Allah swt ! Mjaalie elimu ya Dini
na mfanye mfasiri wa Kitabu (yaani Qur’an
Tukufu)? Na kwa muujiza, Ibn ‘Abbas
akawa Hibr l umma (Imam wa ‘Ummah),
hiyo ilikuwa ni muujiza mojawapo wa Mtume
Muhammad Mustafa s.a.w.w.
Vivyo hivyo
Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alivyomwombea
Abu Hurairah wakati alipolalamikia udhaifu
wa kukumbuka kwake:
Kama vile
ulivyojionea kuwa Ibn ‘Abbas (R) anatambuliwa
hata na Masahaba wengineo kuwa yeye alikuwa
akiijua taawil (tafsiri) ya Qur’an
Tukufu. Kwa hakika huku ni tofauti na kukariri
! Leo hii tunawaona watu wengi wakikariri
Qur’an Tukufu nzima, lakini haimaanishi
kuwa wao wanajua maana halisi iliyomo.
Al-Imam
‘Ali ibn Abi Talib a.s. ni mtu mwingine
ambaye alisema kuwa hakuna Ayah yoyote katika
Qur’an Tukufu ambayo yeye alikuwa
haijui ilipoteremshwa na sababu ya kuteremshwa
kwake na nini kilichokuwa kikimaanishwa.
Kwa hakika
Masahaba wengi walitambua haya kuhusu Shakhsiyyah
hizi na zipo Ahadith zinazosadikiwa katika
kuthibitisha elimu yao hiyo.
Sasa, tukirejea
kwa Abu Hurairah, sisi hatuoni mahala popote
kuwa Abu Hurairah aliipata kipaji hiki cha
maajabu yoyote baada ya Mtume Muhammad Mustafa
s.a.w.w. kumwombea dua !!!
Vile vile
nitapenda kuongezea usahihisho kuwa Abu
Hurairah baada ya kuishi kwake kwa kipindi
kasoro ya miaka mitatu pamoja na Mtume Muhammad
Mustafa s.a.w.w., hakuhadithia au alijiepusha
na kuzisema Ahadith katika zama za makhalifa
watatu
Abu Hurairah
alianza kuhadithia Hadith hususan katika
kipindi cha Mu’awiyah ibn Abu Sufian
yaani takriban miaka 30 baada ya kifo cha
Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Hivyo yeye
alijiwekea kifuani mwake Hadith hizo 3000
na zaidi kwa kipindi chote hicho bila ya
kumwambia mtu yeyote.
Ushahidi
nilionao ni kwamba Abu Bakr, Umar na ‘Uthman
hawakuruhusu usemaji na uandishi wa Hadith.
Imeripotiwa kuwa Abu Hurairah aliulizwa
iwapo alihadithia Hadith katika zama za
‘Utman bin ‘Affan ? Abu Hurairah
alijibu kuwa yeye asingelithubutu kufanya
hivyo, kwani wao wangalimpiga iwapo angelithubutu
kuhadithia Hadith !!
Kwa hakika
si kosa kuchunguza maisha na mienendo ya
Sahaba yeyote, hususan Abu Hurairah. Kwani
wote hao ni wanaadamu tu ambao wanaweza
kukosea kwa madaraja mbalimbali, na wala
hatusemi kuwa Allah swt hawezi kuwasamehe
makosa yao, iwapo Allah swt mwenyewe ataamua
kufanya hivyo.
Hivyo ni wajibu wetu kutambua wazi kuhusu
wale tunaowafuata iwapo kweli ni waaminifu
ili tusije tukapotoka kwani Allah swt ametujaalia
neema kubwa mno ambayo ni fahamu na akili.
Hivyo iwapo tutawaona kuwa hawafai au wapo
mashakani, basi tujiepushe nao ili tusije
tukaiharibu Akhera yetu.
M W I S
H O
|